Niseme Nini Basi

Niseme Nini Basi
ChoirSt. Joseph Migori
AlbumNitachezacheza
CategoryBikira Maria
ComposerAlfred Ossonga

Niseme Nini Basi Lyrics

 1. { Niseme nini basi juu ya mama Yetu Maria
  (Mama Bikira Maria)
  Mama mpendelevu mama mwenye neema } *2

 2. Wakati wa majaribu, mwombezi wetu ni Maria (Mama yetu)
  Wakati wa mashaka kimbilio letu ni Mama (Maria)
 3. Mama uliyeumbwa, pasipo dhambi ya asili
  Ukamzaa mwanao mkombozi wa walimwengu
 4. Moyo wako wa heri moyo safi moyo mweupe
  Nijalie neema nishinde majaribu yote
 5. Mama wa Mkombozi mnara wetu wa Mbinguni
  Mwangaza wetu sisi tunaosafiri gizani
 6. Shika mkono wangu unionyeshe njia ya kweli
  Nifike kwa Mwanao anakoketi uwinguni