Nitamhimidi Bwana

Nitamhimidi Bwana
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumNikiziangalia Mbingu (vol 18)
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerJohn Mgandu
Views22,333

Nitamhimidi Bwana Lyrics

  1. { Nitamhimidi Bwana,
    Kila wakati sifa zake zi kinywani mwangu } *2
    Katika Bwana nafsi yangu (nafsi yangu) itajisifu
    (itajisifu) wanyenyekevu wasikie wafurahi
    Mtukuzeni Bwana (Bwana) pamoja nami
    (pamoja nami) tuliadhimishe jina lake pamoja
    Bwana nafsi yangu (nafsi yangu) itajisifu
    (itajisifu) wanyenyekevu wasikie wafurahi
    Mtukuzeni Bwana (Bwana) pamoja nami
    (pamoja nami) tuliadhimishe jina lake pamoja

  2. Nalimtafuta Bwana akanijibu
    Akaniponya na hofu zangu zote
  3. Wakamwelekea wakatiwa nuru
    Wala nyuso zao hazitaona haya
  4. Maskini aliita Bwana akasikia
    Akamuokoa na taabu zake zote