Nitamhimidi Bwana
Nitamhimidi Bwana Lyrics
Nitamhimidi Bwana kila wakati
Sifa zake zi kinywani mwangu daima
Nafsi yangu itajisifu kwake Bwana
Wanyenyekevu wasikie wafurahi
- Macho ya Bwana hutazama wenye haki
Masikio yake husikia kilio
Uso wake ni juu ya watenda mabaya
Onjeni muone kuwa Bwana yu mwema
- Walilia naye Bwana akasikia
Akawaponya na akawafuta machozi
Yu karibu kwa waliovunjika moyo
Onjeni muone kuwa Bwana yu mwema
- Mateso ya mwenye haki kweli ni mengi
Lakini Bwana humponya nayo yote
Huhifadhi mifupa yao yote
Onjeni muone kuwa Bwana yu mwema