Nitasema

Nitasema
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumMshike Mshike (Vol 5)
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerMarcus Mtinga
Views6,410

Nitasema Lyrics

  1. { Nitasema, nitasema mimi, nitasema, Mwenyezi Mungu
    Kumbe ndiwe furaha moyoni mwangu } *2
    { Kwa heshima nitakutukuza Mungu wangu,
    Tena kwa ujasiri, nitasimulia matendo yako siku zote } *2

  2. Umeniona ukanihurumia,
    Na kwa upole ukanisaidia,
    Na kwa thamani sana nami naapa,
    Sitaacha kukusifu milele
  3. Ee Bwana mimi ni kitu gani kwako,
    Unitazame hata unikumbuke,
    Nina furaha matumaini makubwa,
    Maana wanijali, sikia
  4. Ee Mungu wangu wewe ni nguvu yangu,
    Mimi muovu nakiri unyonge wangu,
    Ni nani tena aliye kama wewe,
    Na tena wanijali, tazama