Njooni Tuimbe

Njooni Tuimbe
Performed bySt. Joseph Migori
AlbumNimeteuliwa
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerAlfred Ossonga
Views24,760

Njooni Tuimbe Lyrics

  1. { Njooni tuimbe, njoni tucheze
    Njooni tufurahi, mbele zake Bwana
    Piga makofi, piga vigelegele
    Shangilieni Bwana leo asubuhi } *2

  2. Sauti ya kwanza semeni aleluya
    Sauti ya pili tumsifu Yesu Kristu
    Sauti ya tatu na ile ya nne
    Waseme pamoja milele amina
  3. Wamama wote pigeni vigelegele
    Wababa wote vinanda vipigwe sana
    Pigeni filimbi ngoma na kayamba
    Watoto wadogo hoye changamkeni
  4. Mataifa yote njoni mbele za Bwana
    Makabila yote simameni tuimbe
    Nyanyukeni wote pigeni makofi
    Shangwe na nderemo vifijo machezo
  5. Bahari na vitu vyote viijazavyo
    Milima mito na miti shangilieni
    Ndege wa angani na warukeruke
    Wanyama kondeni furahini sana