Njooni Tumfanyie Shangwe
   
    
     
         
          
            Njooni Tumfanyie Shangwe Lyrics
 
             
            
- Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
 Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
 Jiungeni wote tuimbe pamoja
 Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
 Kwa miondoko ya raha na kucheza
 Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
 Kwa ngoma safi tamu na za midundiko
 Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
 (Tumpigie) makofi makofi makofi
 (Tumpigie) makofi makofi makofi
 (Tumpigie) makofi makofi makofi
 makofi
- Bwana ametenda wema wa ajabu -
 Machozi ameyageuza vicheko -
 Tumwimbie leo tumsifu yeye -
 Tukipigapiga vifua kwa maringo -
- Tumpungieni mikono kwa madaha -
 Ajue kwamba leo tumefurahi -
 Na shingo zinesenese kwa midundo -
 Mwili uyumbeyumbe kushoto kulia -
- Watoto nao wabebwe juu juu -
 Wajue kwamba Mungu anawapenda -
 Umati wote urukeruke juu -
 Tusisite Mungu yu katikati yetu -
 
 Makofi makofi makofi makofi *8
 Tumpigie (makofi *4) * 6