Login | Register

Sauti za Kuimba

Njooni Tumfanyie Shangwe Lyrics

NJOONI TUMFANYIE SHANGWE

@ Bernard Mukasa

 1. Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
  Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu
  Jiungeni wote tuimbe pamoja -
  Kwa miondoko ya raha na kucheza -
  Kwa ngoma safi tamu na za midundiko

  (Tumpigie) makofi makofi makofi *3

 2. Bwana ametenda wema wa ajabu -
  Machozi ameyageuza vicheko -
  Tumwimbie leo tumsifu yeye -
  Tukipigapiga vifua kwa maringo -
 3. Tumpungieni mikono kwa madaha -
  Ajue kwamba leo tumefurahi -
  Na shingo zinesenese kwa midundo -
  Mwili uyumbeyumbe kushoto kulia -
 4. Watoto nao wabebwe juu juu -
  Wajue kwamba Mungu anawapenda -
  Umati wote urukeruke juu -
  Tusisite Mungu yu katikati yetu -

  Makofi makofi makofi makofi *8
  Tumpigie (makofi *4) * 6
Njooni Tumfanyie Shangwe
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMMungu Yule
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments