Njooni Tumwabudu Bwana
| Njooni Tumwabudu Bwana | |
|---|---|
|  | |
| Performed by | Thika Catholic | 
| Album | Njooni Tumwabudu | 
| Category | Entrance / Mwanzo | 
| Composer | (traditional) | 
| Video | Watch on YouTube | 
| Views | 22,566 | 
Njooni Tumwabudu Bwana Lyrics
- { Njooni tumwimbie na kumshangilia
 Njooni Tumwabudu Bwana } *2
- Njooni tumjongee, njooni kwa masifu
 Njooni tumwabudu Bwana
- Tumfanyie shangwe, mwamba wa wokovu,
 Njooni tumwabudu Bwana
- Yeye ndiye mfalme, wa wafalme wote
 Njooni tumwabudu Bwana
- Milima ni yake, pia makorongo
 Njooni tumwabudu Bwana
- Bahari ni yake, pia nchi kavu
 Njooni tumwabudu Bwana
- Yeye Mungu wetu, alituumba
 Njooni tumwabudu Bwana
- Sisi ndio watu, wa malisho yake
 Njooni tumwabudu Bwana
 
  
         
                            