Njooni Tumwimbie
| Njooni Tumwimbie | |
|---|---|
| Performed by | Our Lady(Star of the Sea) Kenya Navy | 
| Album | Tumeandamana | 
| Category | Entrance / Mwanzo | 
| Composer | Alfred Ossonga | 
| Views | 12,459 | 
Njooni Tumwimbie Lyrics
- Njooni tumwimbie Bwana wetu - kwa shangwe
 Njooni kwa masifu kwa nderemo - tucheze
 {Njooni tuabudu, njooni tusujudu
 Tupige makofi,
 Mbele zake Bwana, Mungu wa ulimwengu } *2
- Hekalu lake Bwana Mungu linapendeza,
 Nyumbani mwake Bwana mna mengi mazuri
 Ninatamani kuingia nyumbani mwake
 Nikae naye siku zote nyuani mwake
 Nipate heri, mbele za Bwana
- Mapema leo ninabisha lango ee Bwana
 Nifungulie nipokee nipe faraja
 Nimelemewa na mizigo mingi ya dhambi
 Nyumbani mwake Bwana ndiko kuna uzima
 Uzima tele, na usalama
- Twendeni sote kwake Bwana Mungu Mwenyezi
 Twendeni kwake tupeleke maombi yetu
 Tutoe shukrani zetu kwa Mungu Baba
 Tutoe na dhabihu zetu kwake Muumba
 Sadaka zetu, azipokee
- Uhai wetu unatoka kwake Muumba
 Tuimbe sifa zake Mungu siku kwa siku
 Tuyatangaze maajabu yake popote
 Tuseme Bwana ametenda mambo makuu
 Kwa watu wote, milele yote.
 
  
         
                            