Njooni Wapenzi (Easter)
Njooni Wapenzi (Easter) Lyrics
- Njooni wapenzi tufanye shangwe
Mwokozi Bwana amefufuka
Viumbe vyote tufanye shangwe
Mwokozi Bwana amefufuka
Na tufanye shangwe, tuimbe aleluya
Mwokozi Bwana amefufuka
- Leo mapema amefufuka -
Kaburi lake ameliacha -
- Walinzi wake walishtuka -
Wakawa kama wamezimia -
- Kwa ufufuko wako ee Bwana -
Umeturudishia uzima -
- Umewashinda adui zetu -
Mauti kali pia shetani -
- Enzi ni yako ya umilele -
Shukrani sifa na utukufu -
- Hii ndiyo siku iliyofanywa -
Na Mungu nayo ni ya furaha -