Njooni Tumshukuru Mungu Lyrics

NJOONI TUMSHUKURU MUNGU

@ J. C. Shomaly

{ Njooni njooni wote tumshukuru Mungu
Kwa mema mema mengi alotujalia } *2
{Ni mengi - ni mema mengi, haya-hesabiki kamwe
Tumepewa sote kwa ma-penzi yake yeye
Tumlipe nini Bwana ili naye apendezwe nasi
Kwa mema mema mengi alotujalia} *2

 1. Ametuumba akili ya kutambua mema na mabaya
  Ametujaza neema tumtambue,
  Tuishi naye daima milele
 2. Wengine katujalia uwezo na mali tumtumikie
  Na wengine vipaji mbalimbali,
  Ili tutambue uwezo wake.
Njooni Tumshukuru Mungu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Cecilia Zimmerman
ALBUMNitasimulia Matendo (Vol 6)
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments