Nota Mpaka Mbinguni
Nota Mpaka Mbinguni Lyrics
- Tumetafiti tukauliza, maandiko tukafunua
Kutambua watakatifu, wanafanya kazi gani Mbinguni
|s1| Usiku na mchana, jioni na asubuhi
Kiangazi masika mpaka Mbinguni
|s2| Tutamsifu Mungu, tutamwimbia
Watunzi tutampangia nota mpaka mbinguni
|a| Tutamsifu Mungu, tutamwimbia
Watunzi Tutampangia nota mpaka Mbinguni
 |t| Tutamsifu, waimbaji tutamwimbia, watunzi
tutampangia nota mpaka Mbinguni (waumini)
|b| Tutamsifu Mungu, tutamwimbia
Watunzi tutampangia nota mpaka Mbinguni
- Enyi wasomi tuambieni, wanasayansi tujibuni
Katika mambo ya mbinguni, nini kinafanyika duniani
- Tumetambua kule mbinguni, hakuna kwenda ofisini
Wala kumbi za burudani, hata kilimo hakuna lakini
- Kumbe furaha za dunia hii, ni upumbafu ni wazimu
Na anasa za maadili, sisi waimbaji tumeamua
- Waamini wote furahini, makasisi shangilieni
Nanyi watawa jiungeni, kwa waimbaji hakuna matata
- Upendo wake ni wa ajabu, fadhili zake za milele
Huruma yake ni amini, msamaha wake unashangaza