Nyanyukeni Wote
Nyanyukeni Wote Lyrics
- Njooni tucheze mbele zake Bwana, wa mapendo
Njooni tutoe shukrani zetu -siku zote
Kwa shangwe
{ Nyanyukeni wote - tuimbe tumtukuze Bwana
Tuyasimulie - pamoja matendo yake makuu } *2
Mwilio tumekula - asante tunashukuru
Damuyo tumekunywa - asante tunashukuru,
Asante, kwa ukarimu, asante, kwa wema wako,
Asante, Kwa kutulisha, asante,
kwa kutunywesha, asante sana
- Njooni wazee hata na vijana - na watoto
Njooni wamama nanyi wasichana - tufurahi
- Njooni tutoe ushuhuda wetu - hadharani
Njooni tuyatangaze maajabu - yake Bwana
- Njooni katika madhabahu yake - takatifu
Njooni katika sinagogi lake - tumsifu
- Njooni tupate baraka za Bwana - Mungu wetu
Njooni tuishi naye tangu leo - na milele