Ondoka Ewe Bibi Arusi
| Ondoka Ewe Bibi Arusi |
|---|
| Performed by | St. Joseph Migori |
| Album | Uzuri wa Yesu |
| Category | Harusi |
| Composer | Alfred Ossonga |
| Views | 18,600 |
Ondoka Ewe Bibi Arusi Lyrics
Ondoka ewe Bwana harusi, tembea wakuone
Ondoka ewe bibi harusi, tembea kwa maringo
Njoo kwangu nikueleze, neno moja toka moyoni mwangu
{ Nimekuchagua wewe, wewe wangu, wa maisha
Tangu leo, mimi na wewe ni kitu kimoja }*2
- Sikiliza nyimbo nzuri nderemo ngoma vinanda
Haya yote ni kwa ajili yangu, mimi na wewe *2
- Angalia vazi langu lilivyopambwa vizuri
Watu wanatushangilia, siku ya leo *2
- Nimekuja kwako leo, uthibitishe hakika,
Mimi kweli ninakupenda, wewe ni wangu *2
- Tumeacha wale wote tumejifunga pamoja
Mimi na wewe hatutengani, milele yote *2