Onjeni Muone
Onjeni Muone Lyrics
(Onjeni muone kwamba -
Onjeni muone yu mwema *2)
Onjeni Mungu Baba (kweli)
Onjeni muone yu mwema
Onjeni Yesu Kristu (kweli)
Onjeni muone yu mwema
- Jiungeni enyi viumbe Mbinguni na duniani
Tuliadhimishe jina lake Mungu Baba kwa pamoja
Kwa kinanda na filimbi, kwa sauti ya baragumu
Kwa vinubi na zeze na ngoma na nyimbo
- Mtukuzeni Bwana Mungu kweli pamoja nami
Tumshangilie kwa furaha katika hekalu lake
Tafuteni Bwana Mungu naye Bwana atawajibu
Atawaponya wote na dhaabu zenu
- Nitamhimidi Bwana Mungu wangu siku zote
Sifa zake zote zi kinywani mwangu daima
Kwa Bwana Mungu wangu, nafsi yangu itajisifu
Wenye haki wasikie wakafurahi
- Elekezeni macho juu, nanyi mtatiwa nuru
Wala nyuso zenu siku zote kamwe zisione haya
Onjeni Mungu Baba onjeni na Yesu Kristu
Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema