Pamoja na Malaika
Pamoja na Malaika | |
---|---|
Choir | St. Cecilia Mwenge Dsm |
Album | Asante Mama wa Yesu |
Category | Bikira Maria |
Composer | (traditional) |
Source | Dsm Tanzania |
Musical Notes | |
Time Signature | 3 4 |
Music Key | G Major |
Notes | Open PDF |
Pamoja na Malaika Lyrics
-
Pamoja na malaika, Mariamu mama yetu
Kuimba sifazo twataka, zipende nyimbo zetuMaria ee zipokee hizo zako heshima
Twakuimba, twakuomba, utwelekee, Mama -
Mazuri ya ulimwengu, si kitu mbele zako
Hata nyota za uwingu, zavia mbele yako -
Bikira uso mfano, sifazo kuzitaja
Sitoshi haba maneno, kubwa yako daraja
//or//
-
Pamoja na malaika, Maria mama yetu
Kuimba sifazo twataka, zipende nyimbo zetuEe Maria zipokee hizo zako heshima
Twakuimba, twakuomba, utwelekee, Mama -
Bikira usiye mfano, sifazo kuzitaja
Sitoshi haba maneno, kubwa yako daraja -
Uliyejaa neema, na mwingi wa huruma
Duniani tukikwama, watuopoa mama