Pasipo Makosa
| Pasipo Makosa | |
|---|---|
|  | |
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Composer | (traditional) | 
| Video | Watch on YouTube | 
| Views | 34,304 | 
Pasipo Makosa Lyrics
- Pasipo makosa Mkombozi wetu,
 Katika baraza la wakosefu
 Na wote walia asulibiwe,
 Aachwe Baraba na Yesu afe
 Aachwe Baraba na Yesu afe
- Ee Yesu washika msalaba wako,
 Na unakubali kufa juu yake
 Ee Yesu useme sababu gani,
 Ya nini mateso makali hayo?
 Ya nini mateso makali hayo?
- "Ni pendo kwa Baba wa uwinguni,
 Ni huruma yangu kwa wakosefu.
 Ewe mkristu kumbuka mateso yangu,
 Uache makosa, uache dhambi
 Uache makosa, uache dhambi"
Recorded by |several songs
* Dar-es-Salaam Cathedral
* St. Patrick Morogoro
  
 
 
 
  
         
                            