Pasipo Makosa

Pasipo Makosa
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Composer(traditional)
VideoWatch on YouTube

Pasipo Makosa Lyrics

 1. Pasipo makosa Mkombozi wetu,
  Katika baraza la wakosefu
  Na wote walia asulibiwe,
  Aachwe Baraba na Yesu afe
  Aachwe Baraba na Yesu afe
 2. Ee Yesu washika msalaba wako,
  Na unakubali kufa juu yake
  Ee Yesu useme sababu gani,
  Ya nini mateso makali hayo?
  Ya nini mateso makali hayo?
 3. "Ni pendo kwa Baba wa uwinguni,
  Ni huruma yangu kwa wakosefu.
  Ewe mkristu kumbuka mateso yangu,
  Uache makosa, uache dhambi
  Uache makosa, uache dhambi"
Recorded by |several songs * Dar-es-Salaam Cathedral * St. Patrick Morogoro