Posho Langu

Posho Langu
Performed bySt. Anthoney Malindi
AlbumMalindi Kuna Nini
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerAlfred Ossonga
Views6,638

Posho Langu Lyrics

  1. Bwana ndiye fungu la posho langu,
    Na la kikombe changu
    {Wewe unaishika kula yangu,
    Nimemwambia Bwana, Bwana
    Wewe ndiwe Bwana wangu } *2

  2. Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri
    Na mtima wangu, umenifundisha usiku
    Nimemweka Bwana mbele yangu daima
    Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu sitaondoshwa
  3. Kwa hivyo moyo wangu, unafurahi moyo wangu
    Washangilia, nao mwili wangu utakaa
    Kwa kutumaini, Maana wewe Bwana
    Hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu
  4. Utanijulisha njia, njia ya uzima
    Mbele ya uso wako, ziko furaha tele,
    Na katika mkono wako wa kuume
    Mkono wa kuume mna neema ya milele
  5. Mungu nihifadhi mimi, maana nakukimbilia
    Wewe Mungu wangu, Bwana ndiwe Bwana wangu,
    Wewe Bwana ndiwe fungu la posho langu
    Na la kikombe changu wewe unaishika kula yangu