Saa ya Hukumu
Saa ya Hukumu | |
---|---|
Performed by | Maria Mt Mama wa Mungu Musoma |
Album | Nchi Imejaa |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Composer | Marcus Mtinga |
Views | 8,759 |
Saa ya Hukumu Lyrics
Saa ya hukumu yangu imefika,
Na wakati wa kufa kwangu umekaribia
Na kitabu cha kumbukumbu yangu kuwa wazi
Yatakaposomwa matendo niliyotenda
Katika siku za uhai wangu duniani
Ni shimo lenye moto ajabu liko mbele yangu
Ninajua nikitupwa humo uhai kwa heri
Nitakwenda wapi mbona simba wamenizunguka
Ninaangamia Bwana ona ninatapatapa.
Sina msaada Bwana njoo unisaidie- Ona adui zangu, sasa wanashangilia
Hata rafiki zangu pia wamejiunga nao
Wanasubiri kwa hamu waone hukumu yangu
Hata mimi mwenyewe mapigo yananienda mbio
Ninakuungamia Mungu wangu nisamehe makosa yangu
Na ndugu zangu ninaomba radhi nimekosa nimekosa sana - Moto unatisha, ni hatari kila upande
Mwanga umepotea, giza limeshika hatamu
Wanyama wenye njaa ona wanavyofurahia
Na nyoka wenye sumu wanajiandaa kunidaka
Na mimi najua bila wewe nimekwisha Mwokozi wangu
Ee Mungu ninakulilia sikiliza ninavyolalamika - Inuka ee Bwana, ili wote washangae
Nyoosha mkono wako, niokoe ee Mungu wangu
Kwa nguvu zako njoo, ee Bwana sema nitainuka
Hata adui zangu washuhudie huruma yako
Nishike mkono Mungu wangu niokoe naangamia
Ee Bwana mapenzi yako yatimizwe nami nitashukuru
Also recorded by St. Cecilia choir, Zimmerman, Nairobi