Saa ya Hukumu

Saa ya Hukumu
ChoirMaria Mt Mama wa Mungu Musoma
AlbumNchi Imejaa
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerMarcus Mtinga

Saa ya Hukumu Lyrics

Saa ya hukumu yangu imefika,
Na wakati wa kufa kwangu umekaribia
Na kitabu cha kumbukumbu yangu kuwa wazi
Yatakaposomwa matendo niliyotenda
Katika siku za uhai wangu duniani
Ni shimo lenye moto ajabu liko mbele yangu
Ninajua nikitupwa humo uhai kwa heri
Nitakwenda wapi mbona simba wamenizunguka
Ninaangamia Bwana ona ninatapatapa.
Sina msaada Bwana njoo unisaidie

 1. Ona adui zangu, sasa wanashangilia
  Hata rafiki zangu pia wamejiunga nao
  Wanasubiri kwa hamu waone hukumu yangu
  Hata mimi mwenyewe mapigo yananienda mbio
  Ninakuungamia Mungu wangu nisamehe makosa yangu
  Na ndugu zangu ninaomba radhi nimekosa nimekosa sana
 2. Moto unatisha, ni hatari kila upande
  Mwanga umepotea, giza limeshika hatamu
  Wanyama wenye njaa ona wanavyofurahia
  Na nyoka wenye sumu wanajiandaa kunidaka
  Na mimi najua bila wewe nimekwisha Mwokozi wangu
  Ee Mungu ninakulilia sikiliza ninavyolalamika
 3. Inuka ee Bwana, ili wote washangae
  Nyoosha mkono wako, niokoe ee Mungu wangu
  Kwa nguvu zako njoo, ee Bwana sema nitainuka
  Hata adui zangu washuhudie huruma yako
  Nishike mkono Mungu wangu niokoe naangamia
  Ee Bwana mapenzi yako yatimizwe nami nitashukuru

Also recorded by St. Cecilia choir, Zimmerman, Nairobi