Safari ya Mafanikio
Safari ya Mafanikio Lyrics
Safari ya mafanikio ni ngumu sana
Ukiwa na imani haba itakushinda
Unapoianza safari bahari imetulia
Unapata matumaini ya kumaliza salama
Ukifika katikati mambo hubadilika
Ni mawimbi na vikwazo misukosuko mingi
Usikate tamaa, jipe moyo utashinda * 2
- Utapata machukizo na matatizo mengi
Ndiyo hali ya dunia, yote uvumilie
Utapata mitihani, migumu ya maisha
Ndiyo hali ya dunia, yote uvumilie
- Utapata vishawishi vingi vya ulimwengu
Ndiyo hali ya dunia vyote uvumilie
Utapata marafiki wema nao wabaya
Ndiyo hali ya dunia wote wavumilie
- Utapata masumbuko na maradhi ya ajabu
Ndiyo hali ya dunia yote uvumilie
Kaza mwendo ndugu yangu
kaza mwendo kwenye nuru
Songa mbele e Mkristu yote uvumilie