Safari ya Mbinguni
Safari ya Mbinguni | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Habari Tuliyoleta (Vol 6) |
Category | Tafakari |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 13,662 |
Safari ya Mbinguni Lyrics
Safari ya kwenda mbinguni kweli ni ngumu
Safari ina mengi ya kutia uchungu
Hakika si ya mchezo
Lazima upigane na shetani, tamaa isikukalie juu
Moyo wako nao uvumilie, ya dunia yapige teketeke
Manahodha, mabaharia si ngumu kidogo,
Hata si kama ya meli
Rubani nanyi abiria si rahisi sana,
Hata si kama ya ndege- [ b ] Safari ya mbinguni yahitaji moyo mweupe
Lazima ukubali nyenyekea kama mtoto
Safari si ya mchezo - Safari ya mbinguni yahitaji uzitubu dhambi
Lazima ukubali makosa bila kushurutishwa
Safari si ya mchezo - Safari ya mbinguni yahitaji moyo wa upendo
Kupenda watu wote hata pia adui yako
Safari si ya mchezo
Composed by Joseph C. Shomaly during St. Paul's Students choir trip to Kitale.