Safari ya Mbinguni

Safari ya Mbinguni
ChoirSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CategoryTafakari
ComposerJ. C. Shomaly

Safari ya Mbinguni Lyrics

 1. Safari ya kwenda mbinguni kweli ni ngumu
  Safari ina mengi ya kutia uchungu
  Hakika si ya mchezo
  Lazima upigane na shetani, tamaa isikukalie juu
  Moyo wako nao uvumilie, ya dunia yapige teketeke

  Manahodha, mabaharia si ngumu kidogo,
  Hata si kama ya meli
  Rubani nanyi abiria si rahisi sana,
  Hata si kama ya ndege

 2. [ b ] Safari ya mbinguni yahitaji moyo mweupe
  Lazima ukubali nyenyekea kama mtoto
  Safari si ya mchezo
 3. Safari ya mbinguni yahitaji uzitubu dhambi
  Lazima ukubali makosa bila kushurutishwa
  Safari si ya mchezo
 4. Safari ya mbinguni yahitaji moyo wa upendo
  Kupenda watu wote hata pia adui yako
  Safari si ya mchezo