Silegei Nakaza Mwendo
| Silegei Nakaza Mwendo |
|---|
| Alt Title | Nakaza Mwendo |
| Performed by | St. Cecilia Zimmerman |
| Album | Silegei (Vol 4) |
| Category | General |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 15,204 |
Silegei Nakaza Mwendo Lyrics
- Naimbaimba nikikusifu Mungu wangu
Nayahubiri matendo yako Mungu wangu mimi
Nakaza mwendo ili nifike mbinguni
(Ili) Nimuone Mungu pia nao malaika (mimi)
{ Silegei, mimi, silegei, (silegei)
Silegei ninakaza mwendo } *2
- Dunia hii yahuzunisha Mungu wangu
Nahangaika kiumbe wako Mungu wangu, sasa
- Mtu ni nani Bwana wewe umkumbuke
Na binadamu kwanza yeye umwangazie, sasa
- Nipe uwezo nivishinde na vishawishi
Niurudie uso wako ee Mungu wangu, sasa