Simama Imara

Simama Imara
Performed by-
CategoryInjili na Miito (Gospel)
Views33,192

Simama Imara Lyrics

  1. Simama, simama imara, jilinde
    Lilinde, neno lako Bwana imara
    Kesha kila siku uombe, uombe, utasimama

  2. Milima yote na mabonde itayeyuka
    Neno lake Bwana imara, imara -litasimama
  3. Mapendo ya Mungu, tumejaa roho ya kweli
    Imara yetu ndani yake, ndaniye, awe muhuri
  4. Siku za huduma ni chache, tuwe mashujaa
    Roho wa Yesu akaa nasi, kaa nasi mpaka hatima
  5. Katika yote tutashinda, kwa nguvu yake
    Nani aweza kututenga, kutenga, na pendo lake
  6. Heri ashikaye maneno, ya Mungu Mwana
    Naam naja upesi Amina, amina njoo Yesu Bwana