Simameni Watu Wote
Simameni Watu Wote Lyrics
Simameni watu wote leo katika nyumba ya Bwana (wote)
Furahini mbele zake Bwana imbeni nyimbo za shangwe
(shangilieni) { Vigelegele, pigeni makofi hekaluni mwake
Mwimbieni Bwana wimbo mpya 1 ( watu wote ) } *2
- Akina mama wote (hoye hoye), akina baba wote (hoye)
Njooni wote mbele za Bwana, mkiimba nyimbo za shangwe
Njooni wote mbele za Bwana, njooni leo mbarikiwe
- Enyi vijana wote (hoye hoye), enyi wazee wote (hoye)
Njooni wote mbele za Bwana, mkiimba nyimbo za shangwe
Njooni wote mbele za Bwana, njooni leo mbarikiwe
- Ni siku ya furaha (leo leo), ni siku ya injili (leo leo)
Tumshukuru muumba wetu, tumsifu Mwenyezi Mungu
Tumshukuru muumba wetu, tumsifu Mwenyezi Mungu