Simu ya Mbinguni
Simu ya Mbinguni |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Views | 4,555 |
Simu ya Mbinguni Lyrics
Ninayo furaha kuwapa siri ya simu ya mbinguni
Siri ndiyo sala simu ya mbinguni
Inayoaminika pia hiyo dawa ya shida
Siri ndiyo sala simu ya mbinguni
Haina malipo haihitaji umeme
Jambo kuu la muhimu nd'o sala
Njia pekee ya kuongea na Mungu
Sala simu ya mbinguni
- Iwe hata asubuhi -yeye utampata
Hata usiku wa manane pia -
yeye utampata mpigie kwa kusali
- Wakati wa mvua au wa jua -
Umeme uwepo na usiwepo -
- Kadi yake haipungui fedha -
Simu yake haiwekwi umeme -
- Kwake hahitaji mnara -
Hata uwe ndani ya shimo refu -
- Kwa wagonjwa pia na maskini -
Kwa matajiri hata mawaziri