Simulia Sifa
| Simulia Sifa | |
|---|---|
| Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
| Album | Nakaza Mwendo (Vol 19-20) |
| Category | Entrance / Mwanzo |
| Composer | Alpha JB Manota |
| Views | 5,780 |
Simulia Sifa Lyrics
{Simulia sifa zake Mungu
Tangaza maajabu ya Mungu
Kwa viumbe vyote vya dunia} *2
{(Jama) Kweli Mungu ni mkuu
A-tawala mataifa kwa haki yeye kila analolitenda
Kwe-tu ni mapenzi yake Mwenyewe }*2- Tazama dunia ilivyoumbika inavyopendeza
Milima, mabonde, misitu, mito, maziwa na bahari
Mungu ameviumba vyote, hakika vinapendeza
Simulia sifa za Mungu, Mungu wetu wa ajabu - Tazama dunia ilivyoumbika inavyopendeza
Wanyama na ndege samaki wadudu na viumbe vyote
Mungu ameviumba vyote, hakika vinapendeza
Simulia sifa za Mungu, Mungu wetu wa ajabu - Tazama dunia ilivyoumbika inavyopendeza
Katuumba sisi wanadamu kwa sura na mfano wake
Mungu ameviumba vyote, hakika vinapendeza
Simulia sifa za Mungu, Mungu wetu wa ajabu