Sioni Ajabu
| Sioni Ajabu | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Habari Tuliyoleta (Vol 6) |
| Category | Tafakari |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 3,782 |
Sioni Ajabu Lyrics
Sioni ajabu mimi ninapotaja jina la Yesu
Na moyo wangu mimi hautachoka kusema Yesu
Maajabu yeye anatenda ukiomba!
Amini amini usadiki utapona!
/ b / Ukoo wetu na unathibitisha
Yesu ni Mwana wa Mungu, te! na!
Sisi tunamsadiki, ukoo wetu, wetu, Yesu
/ s / Ukoo wetu na unathibitisha, yeye ndiye mteule
Ukoo wetu na unathibitisha, Yesu
/ t / Ukoo wetu na unathibitisha yeye ndiye mtawala
[w] Ukoo fulani mliobaki mwangoja nini
Makabila fulani mliobaki mwangoja nini
Vueni ubinadamu yatupeni yale ya kale
Fumba ufumbue macho hili nalo lisikupite.- Kwa jinsi hii Mungu alipenda ulimwengu
Kamtoa mwanawe wa pekee akatuokoa, tunaamini sisi - Tunaamini alikufa kwa makosa yetu
Tumeokolewa kwa damu yake yenye upendo, tunaamini sisi - Funga usali hakuna litakalomshinda
Hata nywele zako azijua kwa idadi yake, tunaamini sisi