Login | Register

Sauti za Kuimba

Sioni Ajabu Lyrics

SIONI AJABU

@ J. C. Shomaly

Sioni ajabu mimi ninapotaja jina la Yesu
Na moyo wangu mimi hautachoka kusema Yesu
Maajabu yeye anatenda ukiomba!
Amini amini usadiki utapona!

/ b / Ukoo wetu na unathibitisha
Yesu ni Mwana wa Mungu, te! na!
Sisi tunamsadiki, ukoo wetu, wetu, Yesu

/ s / Ukoo wetu na unathibitisha, yeye ndiye mteule
Ukoo wetu na unathibitisha, Yesu

/ t / Ukoo wetu na unathibitisha yeye ndiye mtawala

[w] Ukoo fulani mliobaki mwangoja nini
Makabila fulani mliobaki mwangoja nini
Vueni ubinadamu yatupeni yale ya kale
Fumba ufumbue macho hili nalo lisikupite.

  1. Kwa jinsi hii Mungu alipenda ulimwengu
    Kamtoa mwanawe wa pekee akatuokoa, tunaamini sisi
  2. Tunaamini alikufa kwa makosa yetu
    Tumeokolewa kwa damu yake yenye upendo, tunaamini sisi
  3. Funga usali hakuna litakalomshinda
    Hata nywele zako azijua kwa idadi yake, tunaamini sisi
Sioni Ajabu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CATEGORYTafakari
  • Comments