Sisi Wana wa Dunia

Sisi Wana wa Dunia
Alt TitleUsia wa Mama Maria
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumUsia wa Mama Maria
CategoryBikira Maria
ComposerP. F. Mwarabu
SourceDar-es-Salaam Tanzania
VideoWatch on YouTube

Sisi Wana wa Dunia Lyrics

(Usia wa Mama Maria)

Sisi wana dunia tukumbuke maneno,
aliyosema Bikira Maria
Alipowatokea watoto wa Fatima,
Lucia Francis na Jacinta
Alisema tusali, tusali rosari, tupate amani
Na tuwaombee wale wakosefu wasio na mwombezi
Na wasiomwamini Yesu Mwokozi wamuamini ili waokoke

 1. Mama yetu anahuzunishwa sana,
  na matendo yetu maovu
  Anajua adhabu yetu ijayo,
  hivyo anaona huruma sana
 2. Atusihi tuache dhambi kwa dhati,
  tuache kumkosea Yesu
  Tuyatubu makosa yetu yote,
  ili Bwana atupatie amani
 3. Tusitende maovu na dhambi,
  atusihi mama wa Yesu,
  Tusimkasirishe tena Mungu,
  asije tutupa motoni milele
 4. Ibada ya moyo safi wa Maria,
  tuizingatie daima,
  Tupokee komunio takatifu,
  kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi