Sitawaacha Kama Yatima

Sitawaacha Kama Yatima
ChoirSt. Mary's Kwa Njenga
AlbumSitawaacha Mayatima
CategoryRoho Mtakatifu (Pentecoste)

Sitawaacha Kama Yatima Lyrics

 1. Sitawaacha ninyi kama yatima,
  Sitawaacha ninyi (acha ninyi)
  Asema Bwana ( ee Bwana)
  Naja kwenu mioyo yenu ijae,
  Furaha na amani, asema Bwana
  Naja kwenu mioyo yenu ijae,
  Furaha na amani, asema Bwana
  eeh

 2. Nitawaombea ninyi kwa Baba yangu
  Naye atamtuma -Roho- wa kweli
  Huyo Roho Baba atakayemtuma
  Ndiye atakayewafariji mio-yo-ni
 3. Utukufu ulionipa ee Baba
  Nimewapa na wao -ili- wapate
  Kujua ndiwe peke uliyenituma
  Ukawapenda wao ulivyo-ni-pe-nda
 4. Baba hao ulionipa nataka
  Wawe pamoja nami, -nami- popote
  Popote kutazama utukufu wako
  Utukufu ulionipa, anase-ma - Bwa-na
 5. Baba si hao tu ninawaombea
  Lakini nao wale -watao-niamini
  Wote wawe umoja kama we Baba
  Ulivyo ndani yangu nami nda-ni ya-ko
 6. Sitawaacha nyinyi kama yatima
  Waipeleka roho, -yako- e Baba
  Nawe unaufanya uso wa nchi
  Uso wa nchi upya, anase-ma Bwa-na