Talanta Tulizopewa
Talanta Tulizopewa | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Nakaza Mwendo (Vol 19-20) |
Category | Tafakari |
Composer | A. Manota |
Views | 6,882 |
Talanta Tulizopewa Lyrics
{ Talanta tulizopewa na Mungu (Mwenyezi)
Tuzitumieni kwa kujipatia utakatifu } *2- Kama wewe ni baba wa familia
Au kama wewe ni mama wa familia
Kama wewe ni kasisi kanisani
Au kama wewe mtawa kanisani
Vyema utimize wajibu wako upate utakatifu *2 - Kama wewe ni hakimu toa haki
Au kama wewe askari tenda haki
Usionee wanyonge masikini
Acha rushwa acha dhuluma tenda haki,
Vyema utimize wajibu wako upate utakatifu *2 - Kama wewe dakitari au nesi
Hudumia wagonjwa wote kwa upendo
Mashambani maofisini wajibika
Acha uvivu fanya kazi kwa bidii,
Vyema utimize wajibu wako upate utakatifu*2 - Viongozi na watawala tenda haki
Kumbukeni mtaulizwa na Muumba
Walimu nanyi fundisheni maadili
Nanyi wafanya biashara tenda haki
Tutaulizwa juu ya talanta alizotupa Muumba *2