Tazama Tazama
Tazama Tazama |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Views | 17,857 |
Tazama Tazama Lyrics
{ Tazama tazama ni vyema na vizuri
Ndugu kuishi pamoja kwa umoja } *2
- Mapendo ya Kristu yametuunganisha
Ndugu tuishi pamoja kwa mapendo
- Tumshangilie na tufurahie kwake
Tumche tumpende Mungu mzima Bwana
- Kristu Bwana Mungu tunakuomba leo
Tupe neema tukupende wewe
- Tunapokusanyika kwa pamoja daima
Tuangalie tusitengane tena
* * *
- Mapendo ya Kristu yametuunganisha,
Ndugu kuishi pamoja kwa umoja
- Tuwe na furaha tunapokusanyika,
Kwa moyo mnyofu tusameheane kweli,
- Na tuangalie tusitengane kamwe,
Tuache ugomvi tujenge mapatano
- Kati yetu sisi akae Yesu Kristu,
Yeye ni kiungo cha wanadamu wote,
- Awaunganishe waliotengana nasi,
Tuwe kundi moja mchungaji ndiye mmoja.
- Tunapokusanyika kwa pamoja
Tuangalie tusitengane tena
- Kristu Bwana Mungu tunakuomba leo
Tumiminie neema ya kupendana
- Kanisa letu na yale ya wenzetu
Tuungane pamoja tunakuomba