Tazama Tazama

Tazama Tazama
ChoirTBA
CategoryTafakari
Skiza sms 7482442 to 811

Tazama Tazama Lyrics

{ Tazama tazama ni vyema na vizuri
Ndugu kuishi pamoja kwa umoja } *2

 1. Mapendo ya Kristu yametuunganisha
  Ndugu tuishi pamoja kwa mapendo
 2. Tumshangilie na tufurahie kwake
  Tumche tumpende Mungu mzima Bwana
 3. Kristu Bwana Mungu tunakuomba leo
  Tupe neema tukupende wewe
 4. Tunapokusanyika kwa pamoja daima
  Tuangalie tusitengane tena

  * * *
 5. Mapendo ya Kristu yametuunganisha,
  Ndugu kuishi pamoja kwa umoja
 6. Tuwe na furaha tunapokusanyika,
  Kwa moyo mnyofu tusameheane kweli,
 7. Na tuangalie tusitengane kamwe,
  Tuache ugomvi tujenge mapatano
 8. Kati yetu sisi akae Yesu Kristu,
  Yeye ni kiungo cha wanadamu wote,
 9. Awaunganishe waliotengana nasi,
  Tuwe kundi moja mchungaji ndiye mmoja.
 10. Tunapokusanyika kwa pamoja
  Tuangalie tusitengane tena
 11. Kristu Bwana Mungu tunakuomba leo
  Tumiminie neema ya kupendana
 12. Kanisa letu na yale ya wenzetu
  Tuungane pamoja tunakuomba

Favorite Catholic Skiza Tunes