Tazama Wazazi
Tazama Wazazi | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Habari Tuliyoleta (Vol 6) |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 3,747 |
Tazama Wazazi Lyrics
- Tazama wazazi wazuri nilio nao
Ni baba na mama walioyatenda haya
Nidhamu na sala wamenifundisha kwa bidii
Mapendo na wema wamenipa toka utotoni
Sasa nitaimba nimsifu Mungu kwa zawadi hii
Kwa zawadi hii ya wazazi alionipaNikifikiria kiumbe wa Mungu mimi
Nikifikiria ukuu wa Mungu kwangu
Nikitafakari na matendo, anayotenda
Kwa maisha yangu na wazazi, na ndugu zangu
Ninashindwa kuyaelezea kwa kinywa changu
Nitakaa kwake niyatafakari haya - Tazama tazama elimu niliyo nayo
Kumbuka wengine hakujaliwa hiyo
Kwa nguvu ya neno na roho wake mtakatifu
Kanipa nafasi ili nitumike kwa wengine
Sasa nitaimba nimsifu Mungu kwa zawadi hii
Kwa zawadi hii ya elimu aliyonipa - Tazama tazama nchi hii nzuri nilimo
Wengine za kwao hazina amani kamwe
Amani furaha upendo na ukarimu huu
uzuri wa watu wa mito milima na mabonde
Sasa nitaimba nimsifu Mungu kwa zawadi hii
Kwa zawadi hii ya nchi nilimozaliwa