Tazameni Miujiza
Tazameni Miujiza | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Tazameni Miujiza (Vol 2) |
Category | Entrance / Mwanzo |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 7,415 |
Tazameni Miujiza Lyrics
Tazameni miujiza ya Mungu, tazameni maajabu,
Anayotutendea, viumbe tuishio duniani
Katuumba sura mfano wake, mwili wenye kupendeza,
Akili ya maarifa yenye utashi wa kila namna
Nafikiri mimi ninafikiri, Bwana ni nani ni nani ni nani,
Ni nani, ni nani, aliye sawa na wewe Muumba
{Tumpigie makofi, shangwe, watu wote, leo ni shangwe,
Ufukweni mwa bahari, tuimbe wote tumtukuze Mungu } *2- Nafikiri nafikiri, mimi nimeumbwa vipi,
Maajabu yake Mungu, kaniumba mi nilivyo - Dunia ilivyoumbwa, ni kweli Inashangaza,
Yenye wanyama mimea na ardhi yenye rutuba - Nashukuru ee Mungu, kwa mema uliyonipa,
Milele hata milele, utukuzwe Mungu wangu