Tukipenda Wenzetu

Tukipenda Wenzetu
Performed by-
CategoryTafakari
Composer(traditional)
Views22,958

Tukipenda Wenzetu Lyrics

  1. Tukipenda wenzetu, kati yetu Mungu yupo *2

  2. Aliyetufanya tuwe ndugu ndiye Yesu ndugu yetu
    Chuki yote na hasira, kati yetu ziondoe
  3. Tukimpenda Mungu wetu, tuwaze na nduguze
    Audhiye mmoja wao, mapendoye si ya kweli
  4. Tuwe moyo mmoja, roho moja, tuwe pia kundi moja
    Tupendane kama vile Yesu alivyotuvyotupenda
  5. Furahini nyote binadamu, mwimbieni Mungu wenu
    Amri yake ni nyepesi, neno lake kupendana
  6. Kati ya ugomvi na fitina, na katika kisirani
    Mungu wetu hapapendi, Mungu wetu wa amani
  7. Yesu Kiongozi wetu, kweli nenole twalijua
    Jaza nyoyo za wakristu wapendane siku zote