Tukuzeni Jina Lake

Tukuzeni Jina Lake
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumIkatetemeka Nchi (Vol 3)
CategoryZaburi
ComposerD. Wasonga
Views4,144

Tukuzeni Jina Lake Lyrics

  1. Tukuzeni Jina lake, milele na milele *2
    Hubirini kwa watu ajabu zake zote
    Semeni Bwana Mungu ni Bwana wa mabwana
    { Tangazeni kwa kuimba, kwa zaburi hata vinanda,
    Na tarumbeta pia vinubi vyenye sauti ya kupendeza
    Semeni ya kuwa ni Mfalme wa wafalme } *2

  2. Mpeni Bwana utukufu,
    Na nguvu pia mpeni, mwabuduni kwa uzuri wake,
    Kwa uzuri wa utakatifu, tetemekeeni mbele zake
  3. Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
    Mwimbieni Bwana wimbo mpya kwa maana ametenda
    Ametenda mambo ya ajabu machoni pa mataifa
  4. Paazeni sauti zenu,
    Mkiimba kwa furaha, kwa madaha ukirukaruka
    Ukicheza na kusimulia matendo yake ya ajabu