Tumkimbie Shetani Lyrics

TUMKIMBIE SHETANI

Tumkimbie (tumkimbie) huyo huyo shetani (kimbia)
Shetani ameleta mafarakano katika dunia hii *2
Chuki zimetawala ee Bwana, magonjwa ni mengi sana
Tufanye nini tuepuke na matatizo haya *2

 1. Tumeyasahau maagizo ya Bwana wetu Yesu Kristu
  Aliyotufundisha sisi wanadamu, Ndiyo maana kuna machafuko
 2. Mwenye masikio na ayasikilize maneno ya Bwana
  Mkatende kama alivyotenda yeye, Dunia itakuwa na amani
 3. Tungeishi na amani kama samaki katika bahari
  Dunia hii ingekuwa ni paradise, Kama bustani ile ya Edeni
 4. Tumelia sana Bwana hata machozi hayatoki tena
  Tufanye nini sisi ni viumbe wako, Njoo haraka utusaidie
Tumkimbie Shetani
CATEGORYTafakari
 • Comments