Tumsifu Maria

Tumsifu Maria
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumNakupenda Maria
CategoryBikira Maria
Composer(traditional)

Tumsifu Maria Lyrics

 1. Tumsifu Maria, enyi wanae,
  tutoe salamu, tumshangilie

  Salamu, salamu, salamu Maria *2

 2. Nyota ya bahari, mlango wa mbingu
  Mwondoa hatari, mama wa Mungu
 3. Maria bikira, ndiwe mteule
  Umechaguliwa tangu milele
 4. Hakuna mwombaji aombaye
  Kwa Kristu Mwokozi kuliko wewe
 5. Mametu mbinguni tumshangilie
  Mwanao mpenzi pamoja nawe