Tumwangalie Mkombozi

Tumwangalie Mkombozi
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Composer(traditional)
Musical Notes
Time Signature3
4
Music KeyF Major

Tumwangalie Mkombozi Lyrics

 1. Tumwangalie Mkombozi akitundikwa msalabani
  Tutatambua upenzi aliotupenda moyoni.

  { Twimbe, twimbe jamani
  Salaam, Yesu, msalabani } *2

 2. Msalaba sio mtiwe, tunaotaka kuheshimu,
  Ila ni Yesu mwenyewe, kwa binadamu amwaga damu.
 3. Tuusifu sana mti huu, Yesu akauchagulia
  Kwa mapendo yake makuu, deni zetu kuzilipia.
 4. Kwa stahilize msalaba, twapata msamaha wa dhambi
  Ni Yesu mwenye kumwomba Babaye Mungu wetu Rabbi.