Tunaishi Kwa Amani
Tunaishi Kwa Amani Lyrics
(Tunaishi pamoja kwa amani ee ndugu yangu,
Kama jumuiya moja, kwa pendo la Mungu *2)
Ona, {Tumeunganishwa (sote)
Kwa pendo lake Muumba, Sasa,
kwa nini tufarakane
Kwa mambo yatutengayo na Mungu }*2
- Ugomvi kati yetu unatoka wapi,
Mbona sisi sote ni watoto wa Baba mmoja
Kwa nini tugombee mali za dunia
Tukumbuke pendo lake Mungu, tuondoe tofauti zetu
- We baba nawe mama mwagombea nini
Mbona mwasahau ahadi yenu siku ya ndoa
Ugomvi wenu unaathiri watoto
Kumbukeni pendo lake Mungu, muondoe tofauti zenu
- Makasisi, watawa mwatafuta nini
Mbona mwasahau ahadi nazo nadhiri zenu
Ubinadamu mbona unawatawala
Kumbukeni pendo lake Mungu, m'mkabidhi maisha yenu,
- Ugomvi wa kidini unatoka wapi
Mbona sisi sote ni raiya wa taifa moja,
Kubagua kabila, rangi ni kwa nini
Tukumbuke pendo lake Mungu, tuondoe tofauti zetu
- Sasa enyi vijana mwatafuta nini
Mbona matendo yenu mengi ni chukizo kwa Mungu,
Hamuheshimu wazazi na Mungu wenu
Kumbukeni pendo lake Mungu, m'mrudieni Mungu wenu