Login | Register

Sauti za Kuimba

Tupokee Mama Maria Lyrics

TUPOKEE MAMA MARIA

@ P. F. Mwarabu

Tupokee Mama Maria, tuongoze Mama Maria
Tufikishe kwa mwanao Mbinguni

 1. Mama yetu mwema Maria
  Sisi wanao twakukimbilia
  Utusaidie kwa kutuongoza
  Tuweze kuona vyema njia
 2. Tuonee huruma Maria
  Sisi wanao tunaosumbuka
  Utuondolee hofu Maria
  Ya muovu anayetusumbua
 3. Utuelekezee macho yako
  Kwako Yesu Mkombozi Bwana wetu
  Utusamehe dhambi zetu
  Utufikishe Mbinguni kwa Baba
 4. Mama wa Mkombozi Yesu Kristu
  Uwe nasi daima siku zote
  Usituache kamwe peke yetu
  Mpaka Mbinguni tuwe sote
Tupokee Mama Maria
COMPOSERP. F. Mwarabu
CHOIR
CATEGORYBikira Maria
 • Comments