Tutaipataje Amani
| Tutaipataje Amani | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) | 
| Album | Habari Tuliyoleta (Vol 6) | 
| Category | Tafakari | 
| Composer | J. C. Shomaly | 
| Views | 3,872 | 
Tutaipataje Amani Lyrics
- Waumini na mataifa yote na jumuiya zo-te
 Kama chemi chemi mo-ja, na tutafakarini pamoja } *2
 Tutaipataje amani kwa bunduki nayo mabomu
 Tutaipataje amani kwa migogoro ya siasa
 Oooh inasikitisha, tumuombe Mungu atupe hekima
 Oooh enyi mataifa, tumuombe Mungu atupe amani
- Mapanga hata marungu hayatasaidia, kupata amani
 Ugomvi kwa majirani hautasaidia, kupata amani
 Tuweke silaha chini tumuombe Mwenyezi, atupe hekima
 Tukae chini na wenzetu tujadiliane, tupate amani ae
- Makabila kupigana haitasaidia, kupata amani
 Mataifa kupigana haitasaidia, kupata amani
 Mzungu na Mwafrika sisi sote ni ndugu, tuombee amani
 Afrika na Ulaya sisi wana wa Mungu, tuombee amani ae
- Jumuiya mbalimbali tuungane pamoja, tuombee amani
 Afrika Mashariki nayo isiwe nyuma, tuombee amani
 Tanzania nayo Kenya sisi wana wa Mungu, tupendane sote
 Dunia yote sisi sote ni wana wa Mungu, tupendane sote ae
 
  
         
                            