Tutaishia Kusema
Tutaishia Kusema | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | MSHIPI (VOL. 22) |
Category | Tafakari |
Composer | F. Bukene |
Views | 5,338 |
Tutaishia Kusema Lyrics
Tutaishia kusema hii dunia mbaya (kweli) * 2
Mungu kaikamilisha bila kusahau kitu sasa
Dunia iweje mbaya kwa sababu ya walimwengu- Mungu kaumba dunia kwa mpango kamilifu
Kuhakikisha usalama kwa kila alichokiumba
Mazao yanastawi chakula kinatutosha, na mvua
zinanyesha sana kwa sababu ya upendo wake - Wapo walio fukara ambao hawajiwezi
Matajiri hawawasaidii japo wana uwezo
Pia mahospitalini hongo zimeshatawala
Pesa sasa zinatawala kuliko upendo wa Mungu - Viongozi maofisini wananyanyasa raia
Bila hongo hakuna kazi ubinadamu uko wapi
Dunia hii ya leo imetapakaa damu
Silaha za kutisha sana kutwa kucha zafanya kazi