Login | Register

Sauti za Kuimba

Tutaishia Kusema Lyrics

TUTAISHIA KUSEMA

@ F. Bukene

Tutaishia kusema hii dunia mbaya (kweli) * 2
Mungu kaikamilisha bila kusahau kitu sasa
Dunia iweje mbaya kwa sababu ya walimwengu

 1. Mungu kaumba dunia kwa mpango kamilifu
  Kuhakikisha usalama kwa kila alichokiumba
  Mazao yanastawi chakula kinatutosha, na mvua
  zinanyesha sana kwa sababu ya upendo wake
 2. Wapo walio fukara ambao hawajiwezi
  Matajiri hawawasaidii japo wana uwezo
  Pia mahospitalini hongo zimeshatawala
  Pesa sasa zinatawala kuliko upendo wa Mungu
 3. Viongozi maofisini wananyanyasa raia
  Bila hongo hakuna kazi ubinadamu uko wapi
  Dunia hii ya leo imetapakaa damu
  Silaha za kutisha sana kutwa kucha zafanya kazi
Tutaishia Kusema
COMPOSERF. Bukene
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMMSHIPI (VOL. 22)
CATEGORYTafakari
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments