Twendeni kwa Karamu
Twendeni kwa Karamu Lyrics
- Twendeni kwa karamu ya Bwana tumeitwa
Twendeni twende kumpokea
Ni mwaliko wa Bwana
Tukale mkate wa uzima
- Tujitakase mbele ya kwenda kwa karamu hii
Twendeni twende kumpokea
Twende watakatifu
Tukale mkate wa uzima
- Karibu kwangu Yesu ukae kwangu daima
Twendeni twende kumpokea
Nifunze njia yako
Tukale mkate wa uzima
- Na kwa uwezo wako imani yangu naikiri
Twendeni twende kumpokea
We-u Mungu Mwokozi
Tukale mkate wa uzima
- Usituache basi pamoja nasi ukae
Twendeni twende kumpokea
Kwa kuwa kumekucha
Tukale mkate wa uzima
- Na tufurahi mwisho pamwe na Baba milele
Twendeni twende kumpokea
Kwa umoja na Roho
Tukale mkate wa uzima