Twendeni Mezani Mwake
| Twendeni Mezani Mwake | |
|---|---|
| Performed by | - |
| Category | Ekaristia (Eucharist) |
| Views | 8,837 |
Twendeni Mezani Mwake Lyrics
Twende wote mezani mwake
Tukale mwili na kuinywa damu
Ametualika Bwana Yesu kwa karamu- Yesu mwili na damu, chakula safi
Kishibishacho roho zetu
Twendeni sote tukampokee ametualika - Mimi ndicho chakula cha kushibisha
Kilichoshuka kwake Baba
Anayenila ataishi vema siku zote - Alaye chakula kwa kustahili
Hukaa ndani yangu mimi
Nami ndani yake siku zote asema Bwana